English German

Habari katika picha - Ugeni wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani nchini Tanzania

Kikwete na Frank-Walter


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Dkt. Frank-Walter Steinmeier muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo ya faragha huko Ikulu tarehe 25.03.2014.

rais kikwete na waziri wa nje wa ujerumani frank walter pamoja na balozi marmo


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmo na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.

Kikwete, Frank-Walter na wajumbe wengine


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe wakipiga picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na ujumbe aliofuatana nao wakati wakipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.

Text Size

Weather

80°
26°
°F°C
Sunny
Humidity: 80%
28 kph
Wed
Partly Cloudy
73 | 88
22 | 31
Thu
Mostly Sunny
73 | 88
22 | 31